Jumamosi, 31 Desemba 2016

FALSAFA,HISTORIA YA CHAMA CHAA WATAFUTA NJIA



Image result for ADVENTIST YOUTH pathfinder
FALSAFA , HISTORIA YA CHAMA CHA WATAFUTA NJIA.

Chama cha Watafuta Njia ni Kanisa lililojikita zaidi katika mambo ya Kiroho pia huwa na programu za Maburudisho  kwa Vijana wa Umri wa Miaka 10 -15.
Ni mipango na malengo ya Kanisa la Waadventista Wasabato ,linawajibika kuwatengenezea programu zinazowiana na zitakazowavutia Vijana kwa kufanya yafuatayo:
(i)                 Kuwafundisha kwamba Mungu huwapenda na hujali katika maisha yao yote.
(ii)               Kuwatia moyo Watafuta Njia kugundua  kwamba uwezo walionao wamepewa na Mungu na ndiye mtoaji wa vipawa.
(iii)             Kuwatia moyo vijana kwamba wao wanapendwa na Mungu.
(iv)              Kutambua kwamba wokovu ni kwa mtu na ndilo hitaji la Chama.
(v)                Kumjengea Mtafuta Njia kuishi kiafya na kufurahia Uumbaji wa Mungu.
(vi)              Kumfundisha Mtafuta Njia njia ifaayo na mambo yatakayomridhisha  na kufaulu katika maisha yake ya sasa na baadaye.
(vii)            Kuwatia moyo Watafuta Njia kutunza afya zao.
(viii)          Kuwapa nafasi na kuwaandaa katika Uongozi.
(ix)             Kuomba kwa ajili ya kutunza afya zao pamoja na maendeleo ya Kijamii , kiakili na maisha ya kila Mtafuta Njia.

HISTORIA YA CHAMA CHA WATAFUTANJIA.

Kuanzia 1900 – 1907 baadhi ya Makanisa walianzisha Ushirika wa Vijana Wadogo
Mwanzoni mwa 1930 liliingia wazo la kuwa na “ PATHFINDER” katika Calfonia ya Kusini Mashariki  , mwaka uliofuata walifanya Kambi la kwanza huko Bernadin Mountains. Eneo hilo lilinunuliwa kwa ajili ya kufanyia makambi kwa ajili ya shughuli za Vijana  likiwa na ukubwa wa ekari 15  na kuitwa “Junior Missionary Camp”

Mwaka 1930 John Mckim Kiongozi wa Scout aliamua kuanzisha Kikundi cha Vijana Wadogo wa Kanisa la St. Anna . Aliamini kwamba kama Kanisa linahitaji kuwa na kikundi kwa ajili ya mambo ya Kiroho zaidi badala ya shughuliza za Scout. Dr. Theron Johnson alitoa nyumba yake kama sehemu ya kukutania. Nyumba hiyo ipo mpaka leo. Walikutana chini na Wasichana walikutana juu ghorofani na Mrs. Claude Stein alichaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Wasichana na Mume wake walikuwa Washiriki wa Kanisa la Waadaventista Wasabato Fulleston waliamua  kutumia” JINA PATHFINDER”

Mwanzoni mambo yalikwenda vizuri ,lakini baadaye yalibadilika, upinzani ulianza washiriki wengi Kanisa walifikiri kwamba Vijana hawa wanajifunza mambo yasiyoendana na Maadili ya Kiadventista. Shughuli nyingi zilizofanyika wakati ule ni zile zinazofanyika leo na Vijana wetu, kama Michezo, Ukambikaji,na Masomo ya Viumbe vya Asili, Safari za Nje, n.k, lakini muda ulikuwa haujafika kwa Kanisa la St. Anna kuwa na kikundi cha Watafuta Njia.
Baraza la Kanisa lilimtaka Mzee Mckim  na Johnson wavunje kikundi hicho mara moja  vinginevyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao, huduma za Watafuta Njia zilikoma , hadi Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Mwaka 1930 na 1940 Bwana Lawrence Skiner aliamusha wazo la kuwa na Chama cha Watafuta Njia baada ya kuitwa kufanya kazi Kusini Mashariki mwa Calfonia kuwa Mkurugenzi  wa Vijana Wadogo Makanisani, lakini alishauriwa na Jenero Konferensi kuendeleza Jina la JMV badala ya kuanzisha Jina Jipya kama Watafuta Njia. Mwaka 1946 John. H. Harmrock alibuni Nembo yenye sura   ya Pembe Tatu iliyosimamia mambo ya Kiroho ,Kimwili, na Kijamii kulingana na maendeleo ya Mtoto . Utatu Mtakatifu:
                                          Mungu Baba
                                          Mungu Mwana na,
                                          Roho Mtakatifu.

Baadaye Vyama vya Watafuta Njia vilianzishwa katika sehemu za River Side na Glendale vilianzishwa 1946 na 1947 kasi ya uanzishwaji iliongezeka zaidi Mzee Skiner Mkurugenzi  wa Vijana wa Jenero Konferensi aliamini kwamba wakati ulikuwa umefika wa kuanzisha Chama hiki cha pekee na mwaka 1947 -1950 Jina Jipya la Vijana Wadogo toka JMV na kuwa Pathfinder lilifanikiwa zaidi. Mwaka 1950 CHAMA CHA WATAFUTA NJIA kilianzishwa rasmi “Pathfinder lilipitishwa badala ya JMV. Mwaka 1949 --- - - Wakurugenzi wa Vijana walimpendekeza Henry Bergh atayarishe Wimbo wa Watafuta Njia  na mwaka huo huo Wimbo huo ulikuwa  tayari:
                                          Tuwatafuta njia shujaa
                                          Watumishi wa Mungu na
                                          Tu waaminifu wa Kweli
                                          Na  Safi, pia tunao Ujumbe
                                          Unaotukomboa, Yesu Mfalme
                                          Arudi tena kwako nami.

Mwaka 1948 Bwana Henry Bergh alibuni Bendera ya Watafuta Njia na mwaka huo huo Mama Helen Hobbs alishona Bendera ya Kwanza ya Watafuta Njia Lawrence Paulson wa Glendale alibuni na kufaulu kutoa kwa mfululizo Vitabu  kwa ajili ya Vilabu vya Watafuta Njia  pamoja na Shule za Kanisa hii ikijumuisha Mahitaji ya Madarasa ya Vijana. Mwaka 1962  Bwana Clark Smith na Henry Garlick walitunga Mwongozo wa Kwata ( Drill Manuals)
Mwaka 1950 Lawrence Skiner na John Honcock walikutana Washington kwa ajili ya kutayarisha Mwongozo kwa ajili ya Viongozi wa Watafuta  Njia na Mwongozo wa namna ya Kuanzisha  Chama cha Watafuta Njia. Programu na Nembo vilikubaliwa Kiulimwengu  lakini walitumia Lugha tofauti  tofauti kutokana na utafisiri.
                  Nchi zilizoongea Kihisipania walitumia Conquistadors
                  Nchi za Kireno “ Desbravadors”
                  Nchi za Kifaransa walitumia jina la “Enlair”
Programu za Watafuta Njia ziliendelea Maonesho ya Kwanza yalifanyika huko Dinuba, Calfonia Septemba 23,1951.Mwaka 1954 Kamporii ya Kwanza ilifanyika Ulimwenguni. Vyama vya Watafuta Njia vilihudumia wale ambao hawajapevuka , na mwaka 1962 Mkurugenzi wa Vijana wa Kaskazini aliboresha programu ya Watafuta Njia waliopevuka alitumia chama cha Chuo cha Pacific Union kama kielelezo , 1964  Programu ya Watafuta Njia Waliopevuka ya Konferensi ya Calfonia Kusini Mashariki iliimarishwa.






UONGOZI WA WATAFUTA NJIA NGAZI YA JENERO KONFERENSI.


JINA LA MKURUGENZI
MIAKA YA UKURUGENZI

Laurence Skiner
1950 - - 1963

John .H. Hancock
1963 - - 1970

Leo Ranzolin
1970 - - 1980

Mike Stevenson
1980 - - 1986




Malcolm Allen
1986 - - 1997
Robert W. Holborook
1997---- -- -- -- -- ---


KUWAELEWA WATAFUTA NJIA.
Ulinganifu wa pekee unahitajika kwa ajili ya kuwaelewa na kutambua tofauti za  Mahitaji yao ambayo hudhihirisha katika ukuaji wao kufuatana na vipindi vifuatavyo:
                                                  = Pre – Adolesence   9 - 12
                                                   = Ealy Adolesence  13 – 15

                                                 PRE – ADOLESENCE.
Umri wa Vijana  huanzia miaka 9 -12 ni Vijana walio na makelele mengi hawatulii, hawako makini katika kazi zao, ukuaji wao ni wa taratibu sana ,pia huwa  na afya njema , lakini wasichana hukua kwa haraka zaidi kuliko wavulana  pia watu wenye jaziba katika mambo yao mengi. Baada ya miaka 12 huanza kukua kwa haraka na kuanza kurefuka hata miili yao huanza kurefuka hadi kufikia miaka 17 -18. Hiki ni kipindi cha ukuaji huanza kujitegemea kimawazo.

                                                 TABIA ZAO KIAKILI;
(i)                 Vijana wa umri huu hutunza kumbukumbu kama sumaku kwa ajili ya kupokea mambo mapya, Hujifunza kwa haraka na hutunza kile walichojifunza.
(ii)               Ni Vijana wenye bidii  na wachunguzi wa mambo na kujifunza kwayo, hupenda kushika vitu na kujifunza vimetengenezwaje pia hupenda mambo mapya.
(iii)             Wanapenda Masimulizi mapya  na wachunguzi wa Vitabu mbalimbali na kuangalia yaliyomo ndani.
(iv)              Hupenda kukusanya mambo mapya na kuyachunguza. Wataalam wanasema kwamba 90% ya umri huu wa Watoto hujikusanya wanne,watano hujikusanya kulingana na vivutio mahalia ,hiki ni kpindi kizuri cha kuwafundisha Nishani.
(v)                Hiki sio kipindi cha kuchagua mambo maalum bali ni kipindi cha kuwaingiza katika Chama cha Watafuta Njia ,ni kipindi cha uwazi , pia kuwafundisha mambo mapya pamoja  na kutembelea sehemu mbalimbali ,kama vile miezi mitatu kwa ajili ya programu na mwezi mmoja kwa ajili ya Ufundi Stadi.(matembezi kutembelea sehemu mbalimbali)




                                                   TABIA ZA KIMWILI;
(i)                 Wana afya njema.
(ii)               Wana uwiano mzuri wa mawasiliano na akili kama vile michezo,kutembea kwa mwendo mrefu na mambo mbalimbali wanayojifunza.
(iii)             Umri huu  hawawezi kukaa pamoja wakatulia ni muda wa michezo mingi , umri huu ni wa mazoezi mengi mwalimu vyema achague chumba kwa ajili ya kufanya mazoezi kwa ajili ya mapafu, pia wanatakiwa kuwa na shughuli nyingi iwezekanavyo.
(iv)              Hupenda kuiga mambo ya makundi na hutegemea msimamo wa Wazazi kadri wanavyohusiana na Mungu wao.

                                                 MAHUSIANO KIJAMII.
(i)                 Hependa sana kusifiwa na hutunza siri  pamoja na vituko vingi.
(ii)               Hujifunza kwa ushirikiano (kama timu) lakini wana msimamo wa pekee na hulinda imani yake.
(iii)             Ni watukutu sana na huzurura ovyo na wachunguzi na wapelelezi wa mambo na wepesi kuiga tabia za watu ,huiga tabia ya mwalimu ,wazazi.
(iv)              Umri huu  ni wepesi kuamini mwalimu kuliko wazazi wake na hawapendi kuchanganyikana na jinsia nyingine.
(v)                Wavulana hukaa peke yao na Wasichana peke yao.
    
                                                        TABIA ZA KIROHO.
(i)                  Hupenda sana mambo ya Kiroho na kufanya kazi za Kanisa.
(ii)               Ni wakati ufaao na umri mzuri kwa ajili ya Ubatizo hufanya maamzi thabiti kwa kumtafuta Mungu.
(iii)             Umri huu pia ni mashahidi waaminifu na hubiri Injili kwa njia ya matendo yao na maisha yao na hujiweka wakfu kwa Mungu.
(iv)              Ni wepesi kuamini hivyo ni vema pia ni rahisi  kufundisha Dini.

                                       VIJANA WA UMRI WA MIAKA 13 – 15.

                                                 ( EARLY ADOLESENCE)
Kipindi hiki ukuaji wake ni wa haraka pi ni wavivu katika kufanya kazi kwasababu ya uwiano wa akili na mwili, mfadhaiko kwa Vijana wa umri huu husababishwa na baadhi ya viungo kama vile pua , mdomo,na miguu hukua kwa haraka kuliko viungo vingine vya mwili.
Huwafanya wajisikie vibaya husababisha wajione si wa muhimu , pia urefu huanza kupungua na hukoma, badala yake hupenda kuchanganyika na jinsia tofauti wasichana kwa wavulana,  na mapenzi ya ngono huanza.
Kutokana na maendeleo ya akili huweka bayana na husababisha Vijana wa umri huu huanza kuangalia mambo binafsi kuliko kuamini Neno la Mungu kuliko kipindi
kilichopita. Wakati wote ni kipindi hiki ni cha ndoto na huanza kufikiria mambo yajayo kwamba atafanya nini badaye.
Vijana hawa hupenda mambo yanayowapendeza na huwaangalifu nayo ili yasiharibike au mipango yao isiharibike.Changamoto walizo nazo ni kupenda mambo ya starehe ambayo  huchukua nafasi ya mapenzi ya mambo ya Kiroho na huona jambo tu la kawaida  katika mambo ya Mungu.


                                                         TABIA ZA KIAKILI.

(i)                 Ni waangalifu sana na somo kuu katika kipindi hiki , wana ndoto juu ya maisha yajayo kwamba atafanya nini.
(ii)               Hujifunza kwa haraka mambo mapya.
(iii)             Wavulana alimia kubwa hupenda masomo ya Sayansi na masomo mbalimbali na Wasichana hupenda zaidi mabo ya nyumbani.
(iv)              Anahitaji kutambuliwa kwamba anamchango mkubwa katika jamii.
(v)                Huyakubali matendo yake.

                                                           TABIA ZA KIMWILI.
(i)                 wana afya njema mwili wao huvutia.
(ii)               Mwili wao hukua kwa  haraka zaidi na huanza kupenda aina ya  vyakula fulani.
(iii)             Mifupa ya mwili hutanuka ,pia hupoteza mawasiliano kwasababu ya uwiano wa mwili kwasababu umbile alilo nalo na mshipa mkuu hukua kwa haraka.
(iv)              Via vya Uzazi hukua ,mabadiliko  ya kukua hutokea;
Homoni mpya ambayo hukuza via vya Uzazi huathiri tabia ya mhusika kutokana na mabadiliko hayo.  Bwana Rousseau kwamba:
                        tunazaliwa mara mbili , mara ya kwanza huzaliwa kutok
                        a kwa Mama. Na mara ya pili huzaliwa katika maisha am
                        bacho huwa mshirika.
(v)                Wasichana kwa kawaida ni warefu kuliko wavulana wa miaka 12 na 13 ,miaka 14 ni  wembamba na warefu pia miaka 15 na miaka 15 ni miaka 15 vijana wa umri ni wafupi hutofautiana kwa inchi 2 na Vijana wa miaka 16 na wengine hawana tofauti sana na wengine.

                                                                 TABIA ZA KIJAMII.
-Vijana wa umri huu ni waaminifu kwa rika yao ,miongoni mwao ni wacha Mungu.
Hupenda kusifiwa na kutambuliwa na makundi mengine katika shughuli wazifanyazo, Hupendwa kuungwa mkono  na jamii. Uchaguzi wa mambo muhimu huanza katika umri huu.Jambo la pekee katika ni kuwafundisha namna ya kujitambua kabla ya kufikia kwamba ni kipindi cha hatari maishani mwao. Ni vema wafundishwe kazi ya utumishi  kwa ajili ya kazi ya Mungu. Mara nyingi huwa na ukinzani na wasiwasi juu ya maisha yao.