Jumamosi, 19 Agosti 2017

UNABII



FUNGUO ZA KIUNABII
Karama ya Unabii ni moja ya karama za kanisa la kweli la Mungu. Tunasoma katika 2 Petro 1:19-21 ya kuwa kanisa la kristo lina lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo wanadamu watafanya vyema wakiliangalia kwa kuwa ni kama taa ing'aayo mahali penye giza, na kuwawezesha kuiona nuru halisi mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwao.
Lakini kwa namna ya pekee sana Mungu anatutahadharisha kuwa unabii huu unapopatikana katika maandiko haupaswi kufasriwa kwa matakwa yetu kwa jinsi tupendavyo sisi wenyewe. Kwa sababu unabii huu haukuletwa kwetu kwa mapenzi yetu, bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Kwa jinsi hiyo unabii unapaswa ufasriwe kwa kuongozwa na roho Mtakatifu aliye na uwezo wa kutufunulia Kweli Yote.
Jambo la kuzingatia ni kuwa palipo na Roho Mtakatifu ndipo palipo na kweli yote. Kwa hivyo unabii unafasriwa kwa kutumia kweli ambayo kweli ni neno la Mungu. Kwa jinsi hiyo kanuni za kuutafasiri unabii ziko katika Biblia takatifu yenyewe na si kama sisi tupendavyo.

Biblia inatoa funguo zifuatazo katika kufasri unabii wake:

Farasi (horse) Uimara na nguvu ya kivita
Mnyama (beast) Ufalme selikari au mamlaka ya kisiasa
Dubu (bear) Utawala unaoangamiza (Umedi)
Simba (lion) Utawala wenye nguvu nyingi (Babeli)
Chui (leopard) Utawala ulio na kazi ya ajabu (uyunani)
Mwanakondoo (lamb) Yesu Kristo (dhabihu)
Joka (dragon) Shetani na mawakala wake
Nyoka (serpent) Shetani
beberu Uyunani au ugiriki
Kondoo mume Uajemi na umedi
Mbwa mwitu (wolf) Adui
Pembe (horn) Ufalme au mfalme
Mabawa (wings) Spidi, kasi, ulinzi, uokoaji
Hua (dove) Roho Mtakatifu
Mlima (mountains) Utawala wa kisiasa / utawala wa kisiasa na kidini
Mvinyo (Wine) Damu, maagano, mafundisho
Mwanamke bikra (pure woman)= Kanisa la kweli
Mwanamke kahaba (corrupt woman) = Kanisa asi
Kahaba (harlot) Humaanisha dini au kanisa asi
Mavazi/nguo (clothing) Tabia/ matendo
Mavazi meupe (white robes) Matendo ya Haki/ ushindi
Nyota (star) Malaika/ wajumbe
upepo (winds) Huwakilisha mapigano, vita,
Jua (sun) Huwakiisha Yesu / habari njema ya ufalme (injili)
Babeli (Babylon) Mwasi wa imani, machafuko, uasi
Malaika (angel) Mjumbe
Mhuli (seal) Ishara, utambulisho au alama ya kuwatambua watakatifu
mkono (hand) matendo, kazi
Paji la uso (fore head) Akili , kumbukumbu, mawazo
Kichwa (Heads) Tawala, selikari
Alama (mark) Ishara dalili au alama ya kuwatambua waovu

Kwa habari ya rangi na madini kama zilivyotumika kwenye unabii ni kama ifuatavyo:-
Nyeupe (white) Usafi utakatifu
Samawati (blue) Sheria/ amri, mwuaminifu
Nyekundu (red) Kafara, dhambi, rushwa
Zambarau (purple) Cheo/ mamlaka ya kifalme
Dhahabu (gold) Ufalme wa babeli
Fedha (silver) Ufalme wa umedi na uajemi
Shaba (copper) Ufalme wa wayunani
Chuma (iron) Ufalme wa Rumi ya kipagani
Udongo (soil) Ufalme wa Rumi ya kidini
Maji (water) Roho mtakatifu au uzima wa milele
Maji mengi (waters) Eneo linalokaliwa na watu, mataifa
nchi kavu (land) Eneo lisilokaliwa na watu wengi; kinyume cha majimengi; nyika pia hutumika kumaanisha nchi kavu
Moto (fire) Roho Mtakatifu
Taa (lamp) Neno la Mungu
Njaa(famine) Kukosekana kwa ukweli wa Neno la Mungu Amos 8:11

Kwa habari ya kujua muda, majira na nyakati za kiunabii ufunguo ufuatao hutumika;

Siku 1= ina masaa 24 yenye usiku na mchana
Juma 1= lina siku 7 siku sita ziliamriwa ziwe za kazi na siku moja ya saba iwe siku ya mapumziko
Mwezi 1 = una siku 30
Mwaka 1 = una miezi 12
Mwaka 1 = una siku 360 ambazo ni sawa na miezi 12 zidisha kwa siku 30
Biblia inapotaja neno wakati, nyakati mbili na nusu wakati humaanisha yafuatayo:-
Wakati = mwaka 1 = siku 360 = miezi 12
Nyakati mbili = miaka 2 = siku 720 = miezi 24
Nusu wakati = nusu mwaka =siku 180 =miezi 6
Kwa Hesabu hiyo; unabii huo unaposomeka wakati, nyakati mbili na nusu wakati ni sawa na kusema muda wa miaka mitatu na nusu = miezi 42 = siku 1260
Lakini pia katika unabii wa muda mrefu siku 1 = mwaka 1 na kwa mantiki hiyo siku 1260 katika unabii mrefu wa Danieli na ufunuo ni sawa na miaka 1260.

Kwa ufafanuzi zaidi chunguza kwa makini lugha nayotumika katika mafungu yafuatayo:-

Daniel 4:16-36 Moyo wake ubadilike, usiwe moyo wa binadamu, na apewe moyo wa mnyama; nyakati saba zikapite juu yake
v neno nyakati saba ni sawa na miaka 7 mfalme Nebukadneza wa Babeli aliyoishi mwituni

Daniel 7:25, Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati
v maneno wakati, nyakati mbili na nusu wakati ni sawa miaka 3 na nusu =miezi 42 =siku 1260 = na miaka 1260; Daniel 11:13 hufafanua zaidi Daniel 7:25

Ufunuo 12:6 Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini.
v Siku 1260 = miezi 42 = miaka mitatu na nusu = ni miaka 1260

Ufunuo 12:14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.
v Lugha hii ya Ufunuo ya Wakati na nyakati na nusu ya wakati ni sawa kabisa na ile ya Danieli ya wakati nyakati mbili na nusu wakati inayo maanisha miaka 3 na nusu sawa na miezi 42 na sawa na siku 1260 ambazo ni miaka 1260 katika unabii mrefu wa historia ya Dunia

Ufunuo 13:5 Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili
v Miezi 42 *30 =siku 1260 ambazo ni miaka 1260

ndugu msomaji, Kwa utangulizi huu wa unabii, utatusadia kulewa vyema ujumbe wa vitabu vya unabii hususani kitabu cha Danieli na Ufunuo. Bwana akubariki kwa kuupitia somo hili la utangulizi, endelea zaidi kufuatilia masomo yajayo ya kiunabii yatakayotupeleka kuufasri unabii.
Wakati huu tuzame kwa undani zaidi kujua fafanuzi ya hii sanamu aliyoiota mfalme wa  Babeli katika karne ya 7 KK.
Daniel 2:31-35; Wewe, Ee Mfalme, uliona, na tazama, sanamu kubwa sana. Sanamu hii, iliyokuwa kubwa sana, na mwangaza wake mwingi sana, ilisimama mbele yako; na umbo lake lilikuwa lenye kutisha. Na sanamu hii kichwa chake kilikuwa ni cha dhahabu safi; kifua chake na mikono yake ni ya fedha; tumbo lake na viuno vyake ni vya shaba; miguu yake ni ya chuma; na nyayo za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya udongo.  Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande. Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa hari; upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote.

Katika kielelezo hiki cha sanamu aliyoiota Mfalme Nebukadneza ilipata fasiri yake kutoka kwa Dnieli kwa msada wa Roho wa Mungu;
Daniel 2:37-45 Wewe, Ee mfalme, u mfalme wa wafalme, na Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, na uwezo, na nguvu, na utukufu;  na kila mahali wakaapo wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani amewatia mkononi mwako, naye amekumilikisha juu ya hao wote; wewe u kichwa kile cha dhahabu. Na baada ya zamani zako utainuka ufalme mwingine mdogo kuliko wewe; na ufalme mwingine wa tatu wa shaba, utakaoitawala dunia yote. Na ufalme wa nne utakuwa na nguvu mfano wa chuma; kwa maana chuma huvunja vitu vyote na kuvishinda; na kama chuma kisetavyo vitu hivi vyote, ndivyo utakavyovunja-vunja na kuseta. Na kama vile ulivyoziona hizo nyayo za miguu na vidole vyake, kuwa nusu udongo wa mfinyanzi, na nusu chuma, ufalme ule utakuwa ufalme uliogawanyika; lakini ndani yake zitakuwako nguvu za chuma, kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope.  Na kama vidole vya zile nyayo vilikuwa nusu chuma na nusu udongo, kadhalika ufalme ule utakuwa nusu yake una nguvu, na nusu yake umevunjika.

Kichwa cha dhahabu kiliwakilishwa ufalme wa Babylon, yaani Mfalme Nebukadneza. Ufame huuu uliitawalaaa dunia yote kuanzia mwaka 606KK hadi mwaka 539 KK
  
Baada ya utawala huo kuitawala dunia kwa takribani miaka 67, ulifuatiwa na ufalme wa wamedi na waajemi ambao katika sanamu uliwakilishwa kwa kifua na mikono ya fedha.

Utawala wa falme hizi zilizokuwa zimeungana za waamedi na waajemi ulianza mwaka 539 KK na kudumu kwa miaka ipatayo 208 hadi ilipofikia mwaka 331 KK.

Sehemu ya tatu ya sanamu hii ni ile ya kiuno na tumbo vilivyokuwa vya shaba. Ilipotimia mwaka 331 KK, ufalme huu wa waajemi na wamedi ulitekwa na kutawaliwa na Ufalme wa tatu ulioitawala dunia yote pia.
Ufalme huu wa kiuno na tumbo vilivyokuwa na madini ya shaba viliwakilisha utawala wa wayunani. Taifa la Ugriki (Uyunani) walijaliwa kuitawala dunia yote chini ya Mfalme Alexanda Mkuu toka mwaka 331 KK hadi mwaka 168 KK
Baada ya Hizo tawala tatu kupita ulifuatia utawala wa nne wa madini ya chuma. Utawala huu unahusisha miguu yote hadi nyanyo. Lakini jambo la kushangaza ni kuwa nyayo za sanamu japo ni za chuma zenyewe zina mchanganyiko wa udongo. Hii inzfanya kuwepo kwa tofauti na sehemu zingine za miguu kama mapaja maana yenyewe ni chma tu.
Ufalme wa miguu ya chuma uliwakilisha utawala wa Taifa la waroma ulioanza toka mwaka 168 Kabla ya Kristo kuzaliwa na kudumu hadi mwaka  598 Baada ya Kristo Kuzliwa. Hii inatupatia ukweli kuwa Yesu alizaliwa ndani ya utawala wa Waroma kuitawala Dunia

Hizi ndizo tawala nne kuu zilizowahin kuitawala dunia yote. Hata hivyo baada ya tawala hizi nne uliibuka utawala uliokuwa utawala wa nyayo; chuma na udongo. Utawala huu unazuka kutokea miguuni na madini yanayoonekana katika utawala huu ni ya chuma kama ilivyo miguu. Kinachoongezeka Hapa ni udongo. Wanazuoni wa elimu ya kiunabii wanakubaliana wazi kuwa huu utawala hauna budi kuzuka ukitokea Tifa la Rumi kwa sifa zifuatzo:-
1.     Unazuka kutokea Rumi sawasawa na nyayo zinavyozuka zikitokea miguuni
2.    Utawala huu wa nyayo unao vidole 10 ambavyo yanawakilisha mataifa 10 yaliyo
3.    Ufalme unadumu mpaka marejeo ya Kristo
     
  Tofauti na falme zingine zote zilizokuwa na madini ya aina moja, Utawala huu wa nyayo unaundwa kwa aina mbili za madini ambayo hata hivyo hayatashikamana. Utawala huu ndiyo utawala pekee uliowahi kuitawala dunia yote kwa kuunganisha mamlaka ya serikali na mamlaka ya kidini pamoja.
Mwisho wa falme hizi zote na kikomo chazo ni kutokea kwa jiwe kama ilivyotbiliwa katika maandiko, Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.

Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono, na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo, na ile fedha, na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti.

 Hakuna ufalme wowote wa kibinadamu unaoweza kushindana na nguvu za ufame wa Mungu. Jiwe hili limeisambaratisha sanamu hii tikitiki. Matendo 5:29
Tunajifunza historia ya unabii huu ili kuweza kuzitambua majira na kuhesabu vyema siku zetu tuwapo hapa Duniani. Lakini zaidi ya hazo, ni kujua Tumaini pekee alilotundalia Mungu bada ya dhiki na shida za Duniani, Mungu atasimamisha ufalme wake wa milele kwa waliokubali kuitikia wito wake.  Mungu ndiye mwanzilishaji na mhitimishaji wa historia ya dunia yetu hii; Tunapaswa kumsikiliza kwa umakini sana maana yeye ndiye muumbaji na mkombozi wa nafsi za wandamu. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. Tunapata tumaini la ujio wake kwa kuwa imeandikwa; Na tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.

Anakuja upesi kiasi hicho maana alishaahidi kuwa, “Tazama, maskani ya mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. Ujio wa Mwokozi kusimamisha ufalme wake huu ni kwa lengo moja tu kufanya maskani yake pamoja na wanadamu; lakini alituonya mapema kwamba ili afanye maskani nasi sharti tuzingatie kuwa, Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake

Somo hili linakuwa na maana sana pale tunapoamua kuyatoa maisha yetu kwa Kristo. Bwana akubariki.

Jumamosi, 31 Desemba 2016

FALSAFA,HISTORIA YA CHAMA CHAA WATAFUTA NJIA



Image result for ADVENTIST YOUTH pathfinder
FALSAFA , HISTORIA YA CHAMA CHA WATAFUTA NJIA.

Chama cha Watafuta Njia ni Kanisa lililojikita zaidi katika mambo ya Kiroho pia huwa na programu za Maburudisho  kwa Vijana wa Umri wa Miaka 10 -15.
Ni mipango na malengo ya Kanisa la Waadventista Wasabato ,linawajibika kuwatengenezea programu zinazowiana na zitakazowavutia Vijana kwa kufanya yafuatayo:
(i)                 Kuwafundisha kwamba Mungu huwapenda na hujali katika maisha yao yote.
(ii)               Kuwatia moyo Watafuta Njia kugundua  kwamba uwezo walionao wamepewa na Mungu na ndiye mtoaji wa vipawa.
(iii)             Kuwatia moyo vijana kwamba wao wanapendwa na Mungu.
(iv)              Kutambua kwamba wokovu ni kwa mtu na ndilo hitaji la Chama.
(v)                Kumjengea Mtafuta Njia kuishi kiafya na kufurahia Uumbaji wa Mungu.
(vi)              Kumfundisha Mtafuta Njia njia ifaayo na mambo yatakayomridhisha  na kufaulu katika maisha yake ya sasa na baadaye.
(vii)            Kuwatia moyo Watafuta Njia kutunza afya zao.
(viii)          Kuwapa nafasi na kuwaandaa katika Uongozi.
(ix)             Kuomba kwa ajili ya kutunza afya zao pamoja na maendeleo ya Kijamii , kiakili na maisha ya kila Mtafuta Njia.

HISTORIA YA CHAMA CHA WATAFUTANJIA.

Kuanzia 1900 – 1907 baadhi ya Makanisa walianzisha Ushirika wa Vijana Wadogo
Mwanzoni mwa 1930 liliingia wazo la kuwa na “ PATHFINDER” katika Calfonia ya Kusini Mashariki  , mwaka uliofuata walifanya Kambi la kwanza huko Bernadin Mountains. Eneo hilo lilinunuliwa kwa ajili ya kufanyia makambi kwa ajili ya shughuli za Vijana  likiwa na ukubwa wa ekari 15  na kuitwa “Junior Missionary Camp”

Mwaka 1930 John Mckim Kiongozi wa Scout aliamua kuanzisha Kikundi cha Vijana Wadogo wa Kanisa la St. Anna . Aliamini kwamba kama Kanisa linahitaji kuwa na kikundi kwa ajili ya mambo ya Kiroho zaidi badala ya shughuliza za Scout. Dr. Theron Johnson alitoa nyumba yake kama sehemu ya kukutania. Nyumba hiyo ipo mpaka leo. Walikutana chini na Wasichana walikutana juu ghorofani na Mrs. Claude Stein alichaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Wasichana na Mume wake walikuwa Washiriki wa Kanisa la Waadaventista Wasabato Fulleston waliamua  kutumia” JINA PATHFINDER”

Mwanzoni mambo yalikwenda vizuri ,lakini baadaye yalibadilika, upinzani ulianza washiriki wengi Kanisa walifikiri kwamba Vijana hawa wanajifunza mambo yasiyoendana na Maadili ya Kiadventista. Shughuli nyingi zilizofanyika wakati ule ni zile zinazofanyika leo na Vijana wetu, kama Michezo, Ukambikaji,na Masomo ya Viumbe vya Asili, Safari za Nje, n.k, lakini muda ulikuwa haujafika kwa Kanisa la St. Anna kuwa na kikundi cha Watafuta Njia.
Baraza la Kanisa lilimtaka Mzee Mckim  na Johnson wavunje kikundi hicho mara moja  vinginevyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao, huduma za Watafuta Njia zilikoma , hadi Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Mwaka 1930 na 1940 Bwana Lawrence Skiner aliamusha wazo la kuwa na Chama cha Watafuta Njia baada ya kuitwa kufanya kazi Kusini Mashariki mwa Calfonia kuwa Mkurugenzi  wa Vijana Wadogo Makanisani, lakini alishauriwa na Jenero Konferensi kuendeleza Jina la JMV badala ya kuanzisha Jina Jipya kama Watafuta Njia. Mwaka 1946 John. H. Harmrock alibuni Nembo yenye sura   ya Pembe Tatu iliyosimamia mambo ya Kiroho ,Kimwili, na Kijamii kulingana na maendeleo ya Mtoto . Utatu Mtakatifu:
                                          Mungu Baba
                                          Mungu Mwana na,
                                          Roho Mtakatifu.

Baadaye Vyama vya Watafuta Njia vilianzishwa katika sehemu za River Side na Glendale vilianzishwa 1946 na 1947 kasi ya uanzishwaji iliongezeka zaidi Mzee Skiner Mkurugenzi  wa Vijana wa Jenero Konferensi aliamini kwamba wakati ulikuwa umefika wa kuanzisha Chama hiki cha pekee na mwaka 1947 -1950 Jina Jipya la Vijana Wadogo toka JMV na kuwa Pathfinder lilifanikiwa zaidi. Mwaka 1950 CHAMA CHA WATAFUTA NJIA kilianzishwa rasmi “Pathfinder lilipitishwa badala ya JMV. Mwaka 1949 --- - - Wakurugenzi wa Vijana walimpendekeza Henry Bergh atayarishe Wimbo wa Watafuta Njia  na mwaka huo huo Wimbo huo ulikuwa  tayari:
                                          Tuwatafuta njia shujaa
                                          Watumishi wa Mungu na
                                          Tu waaminifu wa Kweli
                                          Na  Safi, pia tunao Ujumbe
                                          Unaotukomboa, Yesu Mfalme
                                          Arudi tena kwako nami.

Mwaka 1948 Bwana Henry Bergh alibuni Bendera ya Watafuta Njia na mwaka huo huo Mama Helen Hobbs alishona Bendera ya Kwanza ya Watafuta Njia Lawrence Paulson wa Glendale alibuni na kufaulu kutoa kwa mfululizo Vitabu  kwa ajili ya Vilabu vya Watafuta Njia  pamoja na Shule za Kanisa hii ikijumuisha Mahitaji ya Madarasa ya Vijana. Mwaka 1962  Bwana Clark Smith na Henry Garlick walitunga Mwongozo wa Kwata ( Drill Manuals)
Mwaka 1950 Lawrence Skiner na John Honcock walikutana Washington kwa ajili ya kutayarisha Mwongozo kwa ajili ya Viongozi wa Watafuta  Njia na Mwongozo wa namna ya Kuanzisha  Chama cha Watafuta Njia. Programu na Nembo vilikubaliwa Kiulimwengu  lakini walitumia Lugha tofauti  tofauti kutokana na utafisiri.
                  Nchi zilizoongea Kihisipania walitumia Conquistadors
                  Nchi za Kireno “ Desbravadors”
                  Nchi za Kifaransa walitumia jina la “Enlair”
Programu za Watafuta Njia ziliendelea Maonesho ya Kwanza yalifanyika huko Dinuba, Calfonia Septemba 23,1951.Mwaka 1954 Kamporii ya Kwanza ilifanyika Ulimwenguni. Vyama vya Watafuta Njia vilihudumia wale ambao hawajapevuka , na mwaka 1962 Mkurugenzi wa Vijana wa Kaskazini aliboresha programu ya Watafuta Njia waliopevuka alitumia chama cha Chuo cha Pacific Union kama kielelezo , 1964  Programu ya Watafuta Njia Waliopevuka ya Konferensi ya Calfonia Kusini Mashariki iliimarishwa.






UONGOZI WA WATAFUTA NJIA NGAZI YA JENERO KONFERENSI.


JINA LA MKURUGENZI
MIAKA YA UKURUGENZI

Laurence Skiner
1950 - - 1963

John .H. Hancock
1963 - - 1970

Leo Ranzolin
1970 - - 1980

Mike Stevenson
1980 - - 1986




Malcolm Allen
1986 - - 1997
Robert W. Holborook
1997---- -- -- -- -- ---


KUWAELEWA WATAFUTA NJIA.
Ulinganifu wa pekee unahitajika kwa ajili ya kuwaelewa na kutambua tofauti za  Mahitaji yao ambayo hudhihirisha katika ukuaji wao kufuatana na vipindi vifuatavyo:
                                                  = Pre – Adolesence   9 - 12
                                                   = Ealy Adolesence  13 – 15

                                                 PRE – ADOLESENCE.
Umri wa Vijana  huanzia miaka 9 -12 ni Vijana walio na makelele mengi hawatulii, hawako makini katika kazi zao, ukuaji wao ni wa taratibu sana ,pia huwa  na afya njema , lakini wasichana hukua kwa haraka zaidi kuliko wavulana  pia watu wenye jaziba katika mambo yao mengi. Baada ya miaka 12 huanza kukua kwa haraka na kuanza kurefuka hata miili yao huanza kurefuka hadi kufikia miaka 17 -18. Hiki ni kipindi cha ukuaji huanza kujitegemea kimawazo.

                                                 TABIA ZAO KIAKILI;
(i)                 Vijana wa umri huu hutunza kumbukumbu kama sumaku kwa ajili ya kupokea mambo mapya, Hujifunza kwa haraka na hutunza kile walichojifunza.
(ii)               Ni Vijana wenye bidii  na wachunguzi wa mambo na kujifunza kwayo, hupenda kushika vitu na kujifunza vimetengenezwaje pia hupenda mambo mapya.
(iii)             Wanapenda Masimulizi mapya  na wachunguzi wa Vitabu mbalimbali na kuangalia yaliyomo ndani.
(iv)              Hupenda kukusanya mambo mapya na kuyachunguza. Wataalam wanasema kwamba 90% ya umri huu wa Watoto hujikusanya wanne,watano hujikusanya kulingana na vivutio mahalia ,hiki ni kpindi kizuri cha kuwafundisha Nishani.
(v)                Hiki sio kipindi cha kuchagua mambo maalum bali ni kipindi cha kuwaingiza katika Chama cha Watafuta Njia ,ni kipindi cha uwazi , pia kuwafundisha mambo mapya pamoja  na kutembelea sehemu mbalimbali ,kama vile miezi mitatu kwa ajili ya programu na mwezi mmoja kwa ajili ya Ufundi Stadi.(matembezi kutembelea sehemu mbalimbali)




                                                   TABIA ZA KIMWILI;
(i)                 Wana afya njema.
(ii)               Wana uwiano mzuri wa mawasiliano na akili kama vile michezo,kutembea kwa mwendo mrefu na mambo mbalimbali wanayojifunza.
(iii)             Umri huu  hawawezi kukaa pamoja wakatulia ni muda wa michezo mingi , umri huu ni wa mazoezi mengi mwalimu vyema achague chumba kwa ajili ya kufanya mazoezi kwa ajili ya mapafu, pia wanatakiwa kuwa na shughuli nyingi iwezekanavyo.
(iv)              Hupenda kuiga mambo ya makundi na hutegemea msimamo wa Wazazi kadri wanavyohusiana na Mungu wao.

                                                 MAHUSIANO KIJAMII.
(i)                 Hependa sana kusifiwa na hutunza siri  pamoja na vituko vingi.
(ii)               Hujifunza kwa ushirikiano (kama timu) lakini wana msimamo wa pekee na hulinda imani yake.
(iii)             Ni watukutu sana na huzurura ovyo na wachunguzi na wapelelezi wa mambo na wepesi kuiga tabia za watu ,huiga tabia ya mwalimu ,wazazi.
(iv)              Umri huu  ni wepesi kuamini mwalimu kuliko wazazi wake na hawapendi kuchanganyikana na jinsia nyingine.
(v)                Wavulana hukaa peke yao na Wasichana peke yao.
    
                                                        TABIA ZA KIROHO.
(i)                  Hupenda sana mambo ya Kiroho na kufanya kazi za Kanisa.
(ii)               Ni wakati ufaao na umri mzuri kwa ajili ya Ubatizo hufanya maamzi thabiti kwa kumtafuta Mungu.
(iii)             Umri huu pia ni mashahidi waaminifu na hubiri Injili kwa njia ya matendo yao na maisha yao na hujiweka wakfu kwa Mungu.
(iv)              Ni wepesi kuamini hivyo ni vema pia ni rahisi  kufundisha Dini.

                                       VIJANA WA UMRI WA MIAKA 13 – 15.

                                                 ( EARLY ADOLESENCE)
Kipindi hiki ukuaji wake ni wa haraka pi ni wavivu katika kufanya kazi kwasababu ya uwiano wa akili na mwili, mfadhaiko kwa Vijana wa umri huu husababishwa na baadhi ya viungo kama vile pua , mdomo,na miguu hukua kwa haraka kuliko viungo vingine vya mwili.
Huwafanya wajisikie vibaya husababisha wajione si wa muhimu , pia urefu huanza kupungua na hukoma, badala yake hupenda kuchanganyika na jinsia tofauti wasichana kwa wavulana,  na mapenzi ya ngono huanza.
Kutokana na maendeleo ya akili huweka bayana na husababisha Vijana wa umri huu huanza kuangalia mambo binafsi kuliko kuamini Neno la Mungu kuliko kipindi
kilichopita. Wakati wote ni kipindi hiki ni cha ndoto na huanza kufikiria mambo yajayo kwamba atafanya nini badaye.
Vijana hawa hupenda mambo yanayowapendeza na huwaangalifu nayo ili yasiharibike au mipango yao isiharibike.Changamoto walizo nazo ni kupenda mambo ya starehe ambayo  huchukua nafasi ya mapenzi ya mambo ya Kiroho na huona jambo tu la kawaida  katika mambo ya Mungu.


                                                         TABIA ZA KIAKILI.

(i)                 Ni waangalifu sana na somo kuu katika kipindi hiki , wana ndoto juu ya maisha yajayo kwamba atafanya nini.
(ii)               Hujifunza kwa haraka mambo mapya.
(iii)             Wavulana alimia kubwa hupenda masomo ya Sayansi na masomo mbalimbali na Wasichana hupenda zaidi mabo ya nyumbani.
(iv)              Anahitaji kutambuliwa kwamba anamchango mkubwa katika jamii.
(v)                Huyakubali matendo yake.

                                                           TABIA ZA KIMWILI.
(i)                 wana afya njema mwili wao huvutia.
(ii)               Mwili wao hukua kwa  haraka zaidi na huanza kupenda aina ya  vyakula fulani.
(iii)             Mifupa ya mwili hutanuka ,pia hupoteza mawasiliano kwasababu ya uwiano wa mwili kwasababu umbile alilo nalo na mshipa mkuu hukua kwa haraka.
(iv)              Via vya Uzazi hukua ,mabadiliko  ya kukua hutokea;
Homoni mpya ambayo hukuza via vya Uzazi huathiri tabia ya mhusika kutokana na mabadiliko hayo.  Bwana Rousseau kwamba:
                        tunazaliwa mara mbili , mara ya kwanza huzaliwa kutok
                        a kwa Mama. Na mara ya pili huzaliwa katika maisha am
                        bacho huwa mshirika.
(v)                Wasichana kwa kawaida ni warefu kuliko wavulana wa miaka 12 na 13 ,miaka 14 ni  wembamba na warefu pia miaka 15 na miaka 15 ni miaka 15 vijana wa umri ni wafupi hutofautiana kwa inchi 2 na Vijana wa miaka 16 na wengine hawana tofauti sana na wengine.

                                                                 TABIA ZA KIJAMII.
-Vijana wa umri huu ni waaminifu kwa rika yao ,miongoni mwao ni wacha Mungu.
Hupenda kusifiwa na kutambuliwa na makundi mengine katika shughuli wazifanyazo, Hupendwa kuungwa mkono  na jamii. Uchaguzi wa mambo muhimu huanza katika umri huu.Jambo la pekee katika ni kuwafundisha namna ya kujitambua kabla ya kufikia kwamba ni kipindi cha hatari maishani mwao. Ni vema wafundishwe kazi ya utumishi  kwa ajili ya kazi ya Mungu. Mara nyingi huwa na ukinzani na wasiwasi juu ya maisha yao.