FUNGUO ZA
KIUNABII
Karama ya Unabii ni moja ya karama za kanisa la kweli la Mungu. Tunasoma katika 2 Petro 1:19-21 ya kuwa kanisa la kristo lina lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo wanadamu watafanya vyema wakiliangalia kwa kuwa ni kama taa ing'aayo mahali penye giza, na kuwawezesha kuiona nuru halisi mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwao.
Lakini kwa namna ya pekee sana Mungu anatutahadharisha kuwa unabii huu unapopatikana katika maandiko haupaswi kufasriwa kwa matakwa yetu kwa jinsi tupendavyo sisi wenyewe. Kwa sababu unabii huu haukuletwa kwetu kwa mapenzi yetu, bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
Kwa jinsi hiyo unabii unapaswa ufasriwe kwa kuongozwa na roho Mtakatifu aliye na uwezo wa kutufunulia Kweli Yote.
Jambo la kuzingatia ni kuwa palipo na Roho Mtakatifu ndipo palipo na kweli yote. Kwa hivyo unabii unafasriwa kwa kutumia kweli ambayo kweli ni neno la Mungu. Kwa jinsi hiyo kanuni za kuutafasiri unabii ziko katika Biblia takatifu yenyewe na si kama sisi tupendavyo.
Biblia inatoa funguo zifuatazo katika kufasri unabii wake:
Farasi (horse) Uimara na nguvu ya kivita
Mnyama (beast) Ufalme selikari au mamlaka ya kisiasa
Dubu (bear) Utawala unaoangamiza (Umedi)
Simba (lion) Utawala wenye nguvu nyingi (Babeli)
Chui (leopard) Utawala ulio na kazi ya ajabu (uyunani)
Mwanakondoo (lamb) Yesu Kristo (dhabihu)
Joka (dragon) Shetani na mawakala wake
Nyoka (serpent) Shetani
beberu Uyunani au ugiriki
Kondoo mume Uajemi na umedi
Mbwa mwitu (wolf) Adui
Pembe (horn) Ufalme au mfalme
Mabawa (wings) Spidi, kasi, ulinzi, uokoaji
Hua (dove) Roho Mtakatifu
Mlima (mountains) Utawala wa kisiasa / utawala wa kisiasa na kidini
Mvinyo (Wine) Damu, maagano, mafundisho
Mwanamke bikra (pure woman)= Kanisa la kweli
Mwanamke kahaba (corrupt woman) = Kanisa asi
Kahaba (harlot) Humaanisha dini au kanisa asi
Mavazi/nguo (clothing) Tabia/ matendo
Mavazi meupe (white robes) Matendo ya Haki/ ushindi
Nyota (star) Malaika/ wajumbe
upepo (winds) Huwakilisha mapigano, vita,
Jua (sun) Huwakiisha Yesu / habari njema ya ufalme (injili)
Babeli (Babylon) Mwasi wa imani, machafuko, uasi
Malaika (angel) Mjumbe
Mhuli (seal) Ishara, utambulisho au alama ya kuwatambua watakatifu
mkono (hand) matendo, kazi
Paji la uso (fore head) Akili , kumbukumbu, mawazo
Kichwa (Heads) Tawala, selikari
Alama (mark) Ishara dalili au alama ya kuwatambua waovu
Kwa habari ya rangi na madini kama zilivyotumika kwenye unabii ni kama ifuatavyo:-
Nyeupe (white) Usafi utakatifu
Samawati (blue) Sheria/ amri, mwuaminifu
Nyekundu (red) Kafara, dhambi, rushwa
Zambarau (purple) Cheo/ mamlaka ya kifalme
Dhahabu (gold) Ufalme wa babeli
Fedha (silver) Ufalme wa umedi na uajemi
Shaba (copper) Ufalme wa wayunani
Chuma (iron) Ufalme wa Rumi ya kipagani
Udongo (soil) Ufalme wa Rumi ya kidini
Maji (water) Roho mtakatifu au uzima wa milele
Maji mengi (waters) Eneo linalokaliwa na watu, mataifa
nchi kavu (land) Eneo lisilokaliwa na watu wengi; kinyume cha majimengi; nyika pia hutumika kumaanisha nchi kavu
Moto (fire) Roho Mtakatifu
Taa (lamp) Neno la Mungu
Njaa(famine) Kukosekana kwa ukweli wa Neno la Mungu Amos 8:11
Kwa habari ya kujua muda, majira na nyakati za kiunabii ufunguo ufuatao hutumika;
Siku 1= ina masaa 24 yenye usiku na mchana
Juma 1= lina siku 7 siku sita ziliamriwa ziwe za kazi na siku moja ya saba iwe siku ya mapumziko
Mwezi 1 = una siku 30
Mwaka 1 = una miezi 12
Mwaka 1 = una siku 360 ambazo ni sawa na miezi 12 zidisha kwa siku 30
Biblia inapotaja neno wakati, nyakati mbili na nusu wakati humaanisha yafuatayo:-
Wakati = mwaka 1 = siku 360 = miezi 12
Nyakati mbili = miaka 2 = siku 720 = miezi 24
Nusu wakati = nusu mwaka =siku 180 =miezi 6
Kwa Hesabu hiyo; unabii huo unaposomeka wakati, nyakati mbili na nusu wakati ni sawa na kusema muda wa miaka mitatu na nusu = miezi 42 = siku 1260
Lakini pia katika unabii wa muda mrefu siku 1 = mwaka 1 na kwa mantiki hiyo siku 1260 katika unabii mrefu wa Danieli na ufunuo ni sawa na miaka 1260.
Kwa ufafanuzi zaidi chunguza kwa makini lugha nayotumika katika mafungu yafuatayo:-
Daniel 4:16-36 Moyo wake ubadilike, usiwe moyo wa binadamu, na apewe moyo wa mnyama; nyakati saba zikapite juu yake
v neno nyakati saba ni sawa na miaka 7 mfalme Nebukadneza wa Babeli aliyoishi mwituni
Daniel 7:25, Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati
v maneno wakati, nyakati mbili na nusu wakati ni sawa miaka 3 na nusu =miezi 42 =siku 1260 = na miaka 1260; Daniel 11:13 hufafanua zaidi Daniel 7:25
Ufunuo 12:6 Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu na mia mbili na sitini.
v Siku 1260 = miezi 42 = miaka mitatu na nusu = ni miaka 1260
Ufunuo 12:14 Mwanamke yule akapewa mabawa mawili ya tai yule mkubwa, ili aruke, aende zake nyikani hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati, mbali na nyoka huyo.
v Lugha hii ya Ufunuo ya Wakati na nyakati na nusu ya wakati ni sawa kabisa na ile ya Danieli ya wakati nyakati mbili na nusu wakati inayo maanisha miaka 3 na nusu sawa na miezi 42 na sawa na siku 1260 ambazo ni miaka 1260 katika unabii mrefu wa historia ya Dunia
Ufunuo 13:5 Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili
v Miezi 42 *30 =siku 1260 ambazo ni miaka 1260
ndugu msomaji, Kwa utangulizi huu wa unabii, utatusadia kulewa vyema ujumbe wa vitabu vya unabii hususani kitabu cha Danieli na Ufunuo. Bwana akubariki kwa kuupitia somo hili la utangulizi, endelea zaidi kufuatilia masomo yajayo ya kiunabii yatakayotupeleka kuufasri unabii.
Wakati huu tuzame kwa undani zaidi kujua fafanuzi ya hii sanamu aliyoiota mfalme wa Babeli katika karne ya 7 KK.

Daniel 2:31-35; Wewe, Ee Mfalme, uliona, na tazama,
sanamu kubwa sana. Sanamu hii, iliyokuwa kubwa sana, na mwangaza wake mwingi
sana, ilisimama mbele yako; na umbo lake lilikuwa lenye kutisha. Na sanamu hii
kichwa chake kilikuwa ni cha dhahabu safi; kifua chake na mikono yake ni ya
fedha; tumbo lake na viuno vyake ni vya shaba; miguu yake ni ya chuma; na nyayo
za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya udongo. Nawe ukatazama hata jiwe
likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake,
iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande. Ndipo kile chuma, na
ule udongo, na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande
vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa hari;
upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga
hiyo sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote.
Katika kielelezo hiki cha sanamu aliyoiota Mfalme
Nebukadneza ilipata fasiri yake kutoka kwa Dnieli kwa msada wa Roho wa Mungu;
Daniel
2:37-45 Wewe, Ee mfalme, u mfalme wa wafalme, na Mungu
wa mbinguni amekupa ufalme, na uwezo, na nguvu, na utukufu; na kila
mahali wakaapo wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani amewatia mkononi
mwako, naye amekumilikisha juu ya hao wote; wewe u kichwa kile cha dhahabu. Na
baada ya zamani zako utainuka ufalme mwingine mdogo kuliko wewe; na ufalme mwingine
wa tatu wa shaba, utakaoitawala dunia yote. Na ufalme wa nne utakuwa na nguvu
mfano wa chuma; kwa maana chuma huvunja vitu vyote na kuvishinda; na kama chuma
kisetavyo vitu hivi vyote, ndivyo utakavyovunja-vunja na kuseta. Na kama vile
ulivyoziona hizo nyayo za miguu na vidole vyake, kuwa nusu udongo wa mfinyanzi,
na nusu chuma, ufalme ule utakuwa ufalme uliogawanyika; lakini ndani yake
zitakuwako nguvu za chuma, kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika na
udongo wa matope. Na kama vidole vya zile nyayo vilikuwa nusu chuma na
nusu udongo, kadhalika ufalme ule utakuwa nusu yake una nguvu, na nusu yake
umevunjika.
Kichwa cha dhahabu kiliwakilishwa ufalme wa
Babylon, yaani Mfalme Nebukadneza. Ufame huuu uliitawalaaa dunia yote kuanzia
mwaka 606KK hadi mwaka 539 KK
Baada ya utawala huo kuitawala dunia kwa takribani
miaka 67, ulifuatiwa na ufalme wa wamedi na waajemi ambao katika sanamu
uliwakilishwa kwa kifua na mikono ya fedha.
Utawala wa falme hizi zilizokuwa zimeungana za
waamedi na waajemi ulianza mwaka 539 KK na kudumu kwa miaka ipatayo 208 hadi
ilipofikia mwaka 331 KK.
Sehemu ya tatu ya sanamu hii ni ile ya kiuno na
tumbo vilivyokuwa vya shaba. Ilipotimia mwaka 331 KK, ufalme huu wa waajemi na
wamedi ulitekwa na kutawaliwa na Ufalme wa tatu ulioitawala dunia yote pia.
Ufalme
huu wa kiuno na tumbo vilivyokuwa na madini ya shaba viliwakilisha utawala wa
wayunani. Taifa la Ugriki (Uyunani) walijaliwa kuitawala dunia yote chini ya
Mfalme Alexanda Mkuu toka mwaka 331 KK hadi mwaka 168 KK
Baada ya Hizo tawala tatu kupita ulifuatia utawala
wa nne wa madini ya chuma. Utawala huu unahusisha miguu yote hadi nyanyo.
Lakini jambo la kushangaza ni kuwa nyayo za sanamu japo ni za chuma zenyewe
zina mchanganyiko wa udongo. Hii inzfanya kuwepo kwa tofauti na sehemu zingine
za miguu kama mapaja maana yenyewe ni chma tu.
Ufalme wa miguu ya chuma uliwakilisha utawala wa
Taifa la waroma ulioanza toka mwaka 168 Kabla ya Kristo kuzaliwa na kudumu hadi
mwaka 598 Baada ya Kristo Kuzliwa. Hii inatupatia ukweli kuwa Yesu
alizaliwa ndani ya utawala wa Waroma kuitawala Dunia
Hizi ndizo tawala nne kuu zilizowahin kuitawala
dunia yote. Hata hivyo baada ya tawala hizi nne uliibuka utawala uliokuwa
utawala wa nyayo; chuma na udongo. Utawala huu unazuka kutokea miguuni na
madini yanayoonekana katika utawala huu ni ya chuma kama ilivyo miguu.
Kinachoongezeka Hapa ni udongo. Wanazuoni wa elimu ya kiunabii wanakubaliana
wazi kuwa huu utawala hauna budi kuzuka ukitokea Tifa la Rumi kwa sifa
zifuatzo:-
1. Unazuka kutokea Rumi sawasawa na nyayo zinavyozuka zikitokea miguuni
2. Utawala huu wa nyayo unao vidole 10 ambavyo yanawakilisha mataifa 10
yaliyo
3. Ufalme unadumu mpaka marejeo ya Kristo
Tofauti na falme zingine zote zilizokuwa na madini ya aina moja, Utawala
huu wa nyayo unaundwa kwa aina mbili za madini ambayo hata hivyo
hayatashikamana. Utawala huu ndiyo utawala pekee uliowahi kuitawala dunia yote
kwa kuunganisha mamlaka ya serikali na mamlaka ya kidini pamoja.
Mwisho wa
falme hizi zote na kikomo chazo ni kutokea kwa jiwe kama ilivyotbiliwa katika
maandiko, Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni
atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine
hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na
kuziharibu, nao utasimama milele na milele.
Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa
mlimani bila kazi ya mikono, na ya kuwa lilivunja-vunja kile chuma, na ile
shaba na ule udongo, na ile fedha, na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu
amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri
yake ni thabiti.
Hakuna
ufalme wowote wa kibinadamu unaoweza kushindana na nguvu za ufame wa Mungu.
Jiwe hili limeisambaratisha sanamu hii tikitiki. Matendo 5:29
Tunajifunza
historia ya unabii huu ili kuweza kuzitambua majira na kuhesabu vyema siku zetu
tuwapo hapa Duniani. Lakini zaidi ya hazo, ni kujua Tumaini pekee alilotundalia
Mungu bada ya dhiki na shida za Duniani, Mungu atasimamisha ufalme wake wa
milele kwa waliokubali kuitikia wito wake. Mungu ndiye mwanzilishaji na
mhitimishaji wa historia ya dunia yetu hii; Tunapaswa kumsikiliza kwa umakini
sana maana yeye ndiye muumbaji na mkombozi wa nafsi za wandamu. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na
mwisho, wa kwanza na wa mwisho. Tunapata tumaini la ujio wake kwa kuwa imeandikwa; Na tazama, naja
upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.
Anakuja
upesi kiasi hicho maana alishaahidi kuwa, “Tazama, maskani ya mungu ni pamoja na wanadamu,
naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye mungu
mwenyewe atakuwa pamoja nao. Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala
mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo
tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. Ujio wa Mwokozi kusimamisha
ufalme wake huu ni kwa lengo moja tu kufanya maskani yake pamoja na wanadamu;
lakini alituonya mapema kwamba ili afanye maskani nasi sharti tuzingatie kuwa, Tazama, naja upesi, na ujira
wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. Heri wazifuao nguo
zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake
Somo hili
linakuwa na maana sana pale tunapoamua kuyatoa maisha yetu kwa Kristo. Bwana
akubariki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni